Arsenal kuvaana na man City Leo usiku - EDUSPORTSTZ

Latest

Arsenal kuvaana na man City Leo usiku

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Licha ya kupunguzwa kasi hivi karibuni na Southampton bosi wa Arsenal, Mikel Arteta amesema wamejipanga kuhakikisha wanapata matokeo mbele ya Manchester City leo Jumatano (April 26).


Arsenal itakua mgeni wa Manchester City katika Uwanja wa Etihad baadae leo Jumatano, huku mchezo huo ukitazamwa kama hatma ya klabu hiyo ya jijini London, katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England.


Mwishoni mwa juma lililopita Arsenal ilikwama mbele ya Southampton baada ya kulazimishwa sare ya mabao 3-3 mchezo ambao ulipigwa Ijumaa (April 21).


Baada ya matokeo hayo, Arsenal imefikisha pointi 75 baada ya michezo 32 huku Man City wakiwa na alama 70 baada ya michezo 30 kwa maana hiyo wana viporo vya michezo miwili.


Kuelekea katika mchezo wa leo dhidi Manchester City, Meneja wa Arsenal Mikel Arteta amesema walifanya makosa katika mchezo uliopita dhidiya Southampton, lakini wachezaji wake walipambana na kuamka tena na anaamini wafanya vizuri leo katika Uwanja wa ugenini.


“Sitaki kusubiri kuna mechi nyingi ambazo tunatakiwa kucheza. Pale mambo yanapokuwa katika hali ngumu ndiyo wakati wa kupambana na kupata matokeo.”


“Tumejiandaa na tumejipanga kwa ajili ya mchezo ujao na hivi ndiyo soka lilivyo kuna wakati unahitaji kuwa katika nafasi fulani, ila mambo yanaenda tofauti. Lakini tumejiandaa kwa ajili ya kwenda kupambana kule Manchester, ” amesema Arteta.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz