Nabi atahadhirisha jambo hili yanga - EDUSPORTSTZ

Latest

Nabi atahadhirisha jambo hili yanga

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Mohamed Nabi amesema bado hawajafuzu nusu fainali ya kombe la Shirikisho la CAF kwani mchezo wao dhidi ya Rivers United haujamalizika, bado kuna dakika nyingine 90 kwenye dimba la Mkapa


Kauli hiyo ya Nabi imekuja baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa kwanza wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Rivers United, ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa bao 2-0, katika Dimba la Godswill Akpabio, mabao yote yakifungwa na Fiston Mayele


"Sisi hatujaja hapa kujifurahisha, nazifahamu timu za Nigeria, kupata matokeo Nigeria ni vigumu sana, lakini tupo serious na mashindano haya. Siku zote nimekuwa nikiwaambia wachezaji wangu wajitahidi kupata matokeo mazuri ugenini kabla ya kuwaza matokeo ya uwanja wa nyumbani, ndicho hicho nilichokifanya"


"Rivers ni timu nzuri, mashindano ya Klabu Bingwa mwaka 2021/22, Rivers walituondoa katika hatua za awali, kulikuwa na sababu nyingi lakini zaidi timu yetu haikuwa kwenye ubora tulionao sasa hivi"


"Sisi Waafrika tunajuana, mechi hii haijaisha, bado kuna mechi nyingine ya marudiano Tanzania baada ya siku saba, kikao changu cha kwanza na wachezaji wangu itakuwa ni kuwasisitiza hilo. Nawaheshimu Rivers, kocha na wachezaji wao wote ni wazuri, lakini sisi tuna malengo ya kufika mbali zaidi kwenye mashindano haya," alisema Nabi



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz