Mlinzi wa kushoto wa Manchester United atema nyongo baada ya kipigo Cha Jana - EDUSPORTSTZ

Latest

Mlinzi wa kushoto wa Manchester United atema nyongo baada ya kipigo Cha Jana

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Mlinzi wa kushoto wa Manchester United amesema kichapo cha 2-0 dhidi ya Newcastle United ni matokeo yasiyokubalika


Aidha Shaw amesema walistahili kupoteza mchezo huo wa ligi kuu ya Premia kwa sababu hawakujituma zaidi ya wapinzani wao


Kikosi cha Erik ten Hag kilishuka hadi nafasi ya nne kwenye jedwali baada ya kichapo hicho cha Newcastle katika mbio za kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao.


Takwimu sio nzuri kwao kwani hawajashinda au kufunga katika mechi zao tatu zilizopita za ligi


"Walipambana zaidi na kuonekana wanauhitaji mchezo zaidi kuliko sisi," Shaw aliambia Sky Sports.


"Sidhani Newcastle walishinda kwa ubora, walishinda kwa hamu, shauku, njaa, mtazamo. Tunahitaji kutambua matatizo yetu haraka na kuibadilisha. Bado tunaweza kuwa na msimu mzuri sana lakini kwa matokeo na uchezaji kama huu, hatuwezi"



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz