Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele, amesema ubora wa kikosi chao unampa imani kubwa ya kufanya vizuri michezo miwili ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na kutinga nusu fainali
Mayele amesema kitendo cha Yanga kufanikiwa kupata pointi kwenye michezo ya ugenini na nyumbani ni ishara nzuri na ubora wa kikosi cha timu hiyo na anaamini watasonga mbele zaidi katika mashindano hayo.
"Malengo yalikuwa ni makundi, lakini tumevuka huko na sasa tunaenda robo fainali, hii ni ishara nzuri kwetu kufanya vizuri na kucheza nusu fainali kwa sababu ya ubora wa kikosi cha timu pamoja na aina ya wachezaji tuliokuwa nao" alisema Mayele.
Aliongeza kuwa wanatambua umuhimu wa michezo iliyopo mbele yao na watafanikisha kila lemgo walilojiwekea na nguvu sasa wanazielekeza katika michezo iliyopo mbele yao hasa huo wa robo fainali.
"Sasa tumerejea nyumbani kujiandaa na michezo iliyopo mbele yetu ya Kombe la Shirikisho la Azam (FA Cup) na ligi kabla hatujacheza michuano ya kimataifa ya hatua ya robo fainali," alisema Mayele
Leo Yanga itafahamu timu itakayochuana nayo katika droo itakayofanyika huko Misri. Pyramids, USM Alger au Rivers United mojawapo itaangukia katika mikono ya Wananchi
Post a Comment