Matokeo Simba vs Ihefu Fc Leo Ijumaa - EDUSPORTSTZ

Latest

Matokeo Simba vs Ihefu Fc Leo Ijumaa

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Mnyama Simba ameunguruma uwanja wa Azam Complex Chamazi, akiibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Ihefu Fc katika mchezo wa robo fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)


Simba ilihitaji dakika 45 tu kumaliza mchezo wakipachika mabao manne huku mshambuliaji Jean Baleke akiendeleza kasi yake ya kuzifumania nyavu akiondoka na mpira baada ya kufunga hat-trik


Baleke sasa amefunga mabao 12 katika mechi tano zilizopita akiwa na wastani wa kufunga zaidi ya mabao mawili katika kila mchezo


Saido Ntibazonkiza naye akaingia kambani akiweka bao la nne huku Pape Ousmane Sakho akiweka bao la tano kwenye dakika za majeruhi


Ihefu Fc walifunga bao lao la kufutia machozi kupitia kwa Raphael Daudi


Katika kipindi cha pili kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira alifanya mabadiliko kwa kuwatoa baadhi ya nyota wake muhimu huku akiwapa nafasi Jonas Mkude, Mohammed Mussa Kennedy Juma na Beno Kakolanya walioingia kuchukua nafasi za Hennock Inonga na Aishi Manula walioumia


Simba sasa imetinga nusu fainali ya michuano hiyo ambapo itachuana na Azam Fc katika mchezo utakaopigwa Nangwanda Sijaona, mkoani Mtwara




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz