Matokeo Mechi za Jana UEFA champions league - EDUSPORTSTZ

Latest

Matokeo Mechi za Jana UEFA champions league

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Mechi za mkondo wa pili robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya zilihitimishwa usiku wa kuamkia leo ambapo Manchester City na Inter Milan zimejihakikishia tiketi ya kutinga nusu fainali zikiungana na AC Milan na Real Madrid


Ikiwa ugenini huko Ujerumani, Man City ilifanikiwa kuitoa Bayern Munich kwa aggregate ya 4-1 baada ya kuilazimisha sare 1-1 katika uwanja wa Allianz Arena


Man City ilishinda mabao 3-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Uingereza


Inter Milan pia wakafuzu kucheza hatua ya nusu fainali kwa kuwaondoa Benfica ya Ureno kwa aggregate ya 5-3 baada ya sare ya mabao 3-3 kwenye mchezo wa mkondo wa pili uliopigwa San Sirro


Inter Milan walishinda mabao 2-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Ureno


Sasa nusu fainali ni AC Milan dhidi ya Inter Milan na Real Madrid dhidi ya Man City, mechi za mkondo wa kwanza zitachezwa Mei 9 2023 na marudiano ni Mei 16 2023.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz