Leo 'kitaeleweka' nchini Morocco wakati Wekundu wa Msimbiazi Simba Sc watakaposhuka uwanja wa Mohammed V kuwakabili wenyeji wao Wydad Athletic katika mchezo wa mkondo wa pili robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Hakuna unyonge kwa Simba kuelekea mchezo huo, baada ya kuishia hatua ya robo fainali mara nne, wakati huu Wanasimba wanasema HAPANA, nusu fainali itawezekana
Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo, ari na morali ya wachezaji wake iko juu, dhamira ni kushinda au kupata matokeo chanya ambayo yataipeleka Simba nusu fainali
Kumekuwa na sintofahamu kuhusu muda wa mchezo lakini sasa ni rasmi mchezo huo utapigwa saa 2 usiku kwa saa za Morocco, kwa muda wa Tanzania ni saa 4 usiku
Ni mechi ngumu lakini kwa hatua ambayo Simba imefika, haipaswi kuhofia kukabiliana na mpinzani aina ya Wydad kwani kwa sasa Simba iko kwenye daraja moja nao kwa kuangalia viwango vya ubora CAF
Simba inaongoza kwa bao 1-0 kutoka ushindi wa mechi ya mkondo wa kwanza, inawezekana kupata ushindi katika mechi ya marudiano leo
No comments:
Post a Comment