Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Licha ya uwanja huo kuelezwa ulishaanza matengenezo madogo madogo huku ukiendelea kutumika kwa mechi kubwa, Mayay amesema kuwa utafungwa baada ya kuanza kwa matengenezo ya eneo la kuchezea.
Amesema matengenezo hayo ya eneo la kuchezea yatasimamiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika 'CAF' kutokana na uwepo wa michuano ya CAF Super Cup
"Sababu kilichokuwa kinafanyika sasa hivi ni matengenezo ya baadhi kama vyumba vya kubadili nguo, maeneo ya wanahabari, vyumba vya waamuzi ambayo ni maboresho madogo lakini yale makubwa yataanza mwezi wa tano ambapo matumizi ya uwanja hayatakuwepo na inatarajia kuwa si chini ya wiki sita mpaka nane," amesema Mayay.
Amesema hayo ni marekebisho ya kawaida kama ilivyoelezwa hapo awali kwani kiwango na ubora wa uwanja hutengenezwa na kutumika kulingana na nyakati husika lakini muda unavyozidi kwenda, inapaswa kufanyiwa maboresho kuendana na nyakati
Kwa maelezo hayo, uwanja huo unaotumika kama uwanja wa nyumbani wa timu za Simba SC na Young Africans, unatarajiwa kutumika na timu hizo kwenye mechi za Robo Fainali za klabu Afrika kabla ya kuanza matengenezo ya eneo la kuchezea.
Na kwa mujibu wa ratiba ya Shirikisho la Soka la Barani Afrika 'CAF' ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mashindano hayo yanatarajiwa kufikia tamati Juni 11, 2023.
No comments:
Post a Comment