Chelsea yamfungashia virago kocha wake mkuu - EDUSPORTSTZ

Latest

Chelsea yamfungashia virago kocha wake mkuu


Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Chelsea imethibitisha kumfuta kazi Graham Potter kama meneja wa klabu hiyo


Kichapo cha 2-0 nyumbani dhidi ya Aston Villa, matokeo ambayo yanawaacha katika nafasi ya 11 kwenye jedwali, kwenye Uwanja wa Stamford Bridge siku ya Jumamosi ilithibitika kuwa mechi ya mwisho ya Potter


Bruno Saltor atachukua mikoba ya kuinoa timu hiyo kama kocha mkuu wa muda huku mechi inayofuata ya Chelsea ikiwakaribisha Liverpool Jumanne usiku.


Aidha, tangazo la kilabu lilipendekeza Potter anaweza kuchukua jukumu katika kuamua ni nani mrithi wake wa kudumu.


"Chelsea FC imetangaza kwamba Graham Potter ameondoka kwenye klabu. Graham amekubali kushirikiana na klabu ili kuwezesha mabadiliko ya haraka"


"Katika wakati wake na klabu, Graham ametupeleka robo fainali ya Ligi ya Mabingwa, ambapo tutamenyana na Real Madrid. Chelsea inapenda kumshukuru Graham kwa juhudi zake zote na mchango wake na kumtakia heri kwa siku zijazo," ilisema taarifa ya ChelseaDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz