"Binafsi natamani kuona Yanga ikifika hata fainali ya michuano hii," Senzo - EDUSPORTSTZ

Latest

"Binafsi natamani kuona Yanga ikifika hata fainali ya michuano hii," Senzo

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Mtendaji Mkuu wa zamani wa Yanga, Senzo Mbatha Mazingiza, amesema anaiona Yanga ikivuka hatua ya nusu fainali na hata kufika mbali zaidi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika kutokana na ubora wa timu yao


Senzo ambaye kwa sasa ni CEO katika Shirikisho la Soka Botswana, amesema kwa kiasi kikubwa ubora ambao wameuonesha Yanga katika Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu, wana uwezo mkubwa wa kusonga mbele katika michuano hiyo


"Yanga mpaka sasa wamecheza vizuri sana, ukiwatazama kwa jinsi ambavyo wameingia robo fainali utabaini ni timu ambayo ina nguvu kubwa sana katika michuano hii"


"Ninaamini watafika mbali zaidi ya walipofika sasa. Uwezo wa kutinga nusu fainali wanao, hata wapinzani ambao watakutana na Yanga katika robo fainali sioni kama wanapaswa kuwapa hofu, wakijipanga vizuri na kucheza kama walivyocheza kwenye makundi, watavuka"


"Binafsi natamani kuona Yanga ikifika hata fainali ya michuano hii," alisema Senzo


Yanga itachuana na Rivers United katika hatua ya robo fainali ambapo mchezo wa kwanza utapigwa April 23 huko Nigeria na marudiano kupigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, April 30Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz