Arsenal nao kama Man City wampiga mtu 4-1 - EDUSPORTSTZ

Latest

Arsenal nao kama Man City wampiga mtu 4-1

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Gabriel Jesus alimaliza ukame wake wa mabao wa miezi sita akifunga mara mbili katika ushindi wa 4-1 wa Arsenal dhidi ya Leeds huko Emirates.

Mshambulizi huyo wa Brazil alikuwa anaanza kwa mara ya kwanza Ligi Kuu ya Uingereza 2023 baada ya kupona kutokana na upasuaji wa goti.

Akianza kikosini nafasi ya Bukayo Saka ambaye ni mgonjwa, Jesus alilipa imani ya Mikel Arteta kumwanzisha

Na ni mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 aliyefungua ukurasa wa mabao kaskazini mwa London, huku Arsenal wakitangulia katika dakika ya 35

Jesus alishinda penalti baada ya kukatwa na beki wa kulia wa zamani wa akademi ya Gunners Luke Ayling na mwenyewe kufunga mkwaju huo wa penati

Lilikuwa ni bao lake la kwanza tangu kufunga katika ushindi wa 3-1 dhidi ya wapinzani wao Tottenham mnamo Oktoba 1 miezi sita iliyopita

Ben White akaiongezea Arsenal bao la pili kabla ya Jesus kuongeza jingine la tatu na Grait Xhaka kuhitimisha bao la nne. Bao pekee la kufutia machozi kwa Leeds lilifungwa na Rasmus Krintensen

Ushindi huo umerejesha gap la pointi baina yake na Manchester City kuwa nane, Arsenal ikiwa imecheza mechi moja zaidiDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz