Ally Kamwe atema Nyongo Kwa wanao ponda kiwango Cha Aziz Ki kushuka - EDUSPORTSTZ

Latest

Ally Kamwe atema Nyongo Kwa wanao ponda kiwango Cha Aziz Ki kushuka

Kupata Kifurushi cha bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amemkingia kifua mchezaji wao, Stephane Aziz Ki kufuatia baadhi ya wachambuzi kudai kuwa ameshuka kiwango.


"Tumebaki na Wachambuzi wachache mno wenye kufahamu misingi ya football, wenye kujua uhalisia wa huu mchezo,wengi wao hata hiyo passion yenyewe hawana, ni vile shughuli za kufanya mjini hakuna, imebidi wavamie fani zisizowahusu.


"Mijadala yao kuhusu @aziz.ki.10 inaprove hilo pasi na shaka, Sijui nani aliwaambia Mcheza mpira anakuwa katika form yake siku zote? Messi? Pele? au Ronaldo?


"Yupi katika hao Mastar wakubwa always anakuwa byee uwanjani? Kama hilo hawalijui huku kwenye football kimewaleta nini ? Dogoli au Mchezo wa Pete ni sehemu yao sahihi inayowafaa kuwepo,Sijui kipi kimewaleta huku!!


"@mayelefiston asipofunga Game mbili tu wanaanza kumponda baadae wanaona aibu,Hawa Hawa Bata Maji ndio waliomponda @lomalisa4 , leo wamenyuti, ni Kuku hawa hawa ndio waliosema @mwamnyeto03 sio beki bora, leo sura zao zinainama chini kama mafisi yaliyofumaniwa ukweni.


"Aziiz You are magician bro, Football ipo hvyo na sio ajabu, nyakati nzuri na mbaya humtokea mchezaji yoyote yule,and this is quite ordinary kwenye life cycle za footballer yoyote yule duniani.


"Prove them wrong haraka na rejesha mind yako kutekeleza Majukumu yako kiufasaha, wewe ni mchezaji mkubwa mno, nitakukumbusha watakaporudi kukuimba tena, hawana haya hao, waliwahi kuchangishana hadi buku buku kumtoa njiani Mayele, sasa hivi na selfie wanaomba nae kisha wanapost bila aibu.


"Kikubwa Wananchi tuendelee kuwaunga mkono Wachezaji wetu katika nyakati zao zote, nzuri na mbaya,ntusikubali kucheza Bit za Mashetani Pori na Kaswende zao Sugu zisizosikia dawa," amesema Kamwe.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz