Yanga waingiza mabilioni haya baada ya kutinga Robo Fainali kombe la shirikisho Africa - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga waingiza mabilioni haya baada ya kutinga Robo Fainali kombe la shirikisho Africa

Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA

Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Baada ya kufanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika, Yanga imejihakikishia kuvuna Tsh Milioni 820 kutoka kwa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF)


Hiyo inafanya Yanga iwe na uhakika wa kuvuna takribani Tsh Bilioni 2.3 katika michuano hiyo hata kama itaishia hatua ya robo fainali


Yanga ina mkataba na kampuni ya Haier wenye thamani ya Tsh Bilioni 1.5 ambao ni maalum kwa ajili ya kombe la Shirikisho


Kama Wananchi watafanikiwa kutinga nusu fainali watavuna Tsh Bilioni 1 kutoka CAF (jumla Tsh Bil 2.5) na kama watatinga fainali watavuna Tsh Bil 1.5 (jumla Tsh Bilioni 3) na ikitokea wametwaa ubingwa wa Shirikisho Wananchi watavuna Tsh Bilioni 3 kutoka CAF na hivyo kukusanya jumla ya Tsh Bilioni 4.5 ikiwa ni pamoja na fedha za Haier


Pia kuna fedha za bonus kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk Samia Suluhu Hassan mpaka sasa Yanga ikivuna Tsh Milioni 40 baada ya kufunga mabao nane


Kwa hakika huu utakuwa msimu bora kwa Yanga katika kukusanya mapato katika mashindano ya CAFDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz