Wachezaji wa Yanga walioingia kwenye kikosi Bora Cha Caf - EDUSPORTSTZ

Latest

Wachezaji wa Yanga walioingia kwenye kikosi Bora Cha Caf


 Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA

Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Mlinzi wa kushoto wa Yanga Joyce Lomalisa ameendelea kuwaborakutokana na kiwango bora anachoonyesha katika kikosi cha Yanga


Kwa sasa unaweza kusema Lomalisa ndiye mchezaji mahiri zaidi upande wa kushoto katika ligi kuu ya NBC


Lomalisa ametajwa kwenye kikosi cha wiki cha CAF kwa michuano ya kombe la Shirikisho sambamba na mshambuliaji Kennedy Musonda


Mcongomani huyo pia alijumuishwa kwenye kikosi cha CAF cha Shirikisho baada ya mechi za raundi ya nne


Utofauti wa Lomalisa na walinzi wengi wa pembeni ni uwezo wake mkubwa wa kupanda na kushuka


Ukiangalia mchezo uliopita dhidi ya US Monastir, Lomalisa ni kama alikuwa akicheza winga akimpa uhuru Kennedy Musonda kuingia ndani kuungana na Fiston Mayele pale timu inaposhambulia


Lomalisa ndiye mchezaji aliyepiga krosi nyingi zaidi katika mchezo huo (7), takwimu zikimuonyesha kuwa mchezaji aliyehusika katika mashambulizi mengi ya Yanga


Wakati mwingine Nabi anaweza kumtumia kama winga na huenda akawa na madhara zaidi akitumika katika nafasi hiyo kutokana na aina yake ya uchezajiDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz