Tetesi za usajili barani ulaya Leo Alhamisi - EDUSPORTSTZ

Latest

Tetesi za usajili barani ulaya Leo Alhamisi


 Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA

Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Arsenal, Chelsea na Manchester City wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Italia Wilfried Gnonto, 19, kutoka Leeds United. (Gazzetta dello Sport, Via Metro)


Juventus na Napoli ni miongoni mwa vilabu kadhaa vya Italia ambavyo pia vinavutiwa na Gnonto. (90min) 0


Manchester United inaweza kutumia hamu ya Tottenham kumnunua mlinda mlango Mwingereza Dean Henderson, 26, kuwashawishi Spurs kumuuza mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, 29. (ESPN)


Mshambulizi wa Eintracht Frankfurt wa Ufaransa Randal Kolo Muani, 24, ambaye analengwa kwa pauni milioni 105 na Manchester United, amependekeza kuwa yuko tayari kuhama msimu huu. (L'Equipe, Via Mail)


Manchester City wamefufua nia yao ya kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Florian Wirtz, 19. (90min)


Tottenham iko kwenye hatari ya kumkosa meneja wa zamani Mauricio Pochettino msimu wa joto huku Muajentina huyo akiwa juu kwenye orodha ya wanaotamani Real Madrid iwapo kocha wa sasa Carlo Ancelotti ataondoka. (Times)


Chelsea wamekubali kwamba watahitaji kupata hasara kubwa ikiwa wanataka kumuuza mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 29, msimu wa joto. (Football Insider)


Matumaini ya Arsenal na Barcelona kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania Martin Zubimendi kutoka Real Sociedad yanaonekana kuisha baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kusema hatarajii kuondoka mwishoni mwa msimu huu. (Mail)


Barcelona wana nia ya kumsajili beki wa Monaco mwenye umri wa miaka 21 Vanderson. (Sport – In Hispanic)


Vilabu kadhaa vimeonyesha nia ya kutaka kumsajili beki wa kushoto Mwingereza Brandon Williams, 22, kutoka Manchester United. (Football Insider)


Kiungo wa kati wa Juventus na Ufaransa Adrien Rabiot, 27, amedokeza kuwa huenda akavutiwa na uhamisho wa kuelekea Liverpool. (Sun)


BBCDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz