TFF yatupilia mbali shauri la Feisal (maombi yake hayana mashiko)
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana leo tarehe 2 Machi, 2023 kwa ajili ya kusikiliza pamoja na mambo mengine shauri la mapitio (Review) ya uamuzi wake wa tarehe 9 Januari 2023 kati ya Feisal Salumu na Klabu ya Young Africans kama yalivyowasilishwa na muombaji Feisal Salum dhidi ya Klabu ya Young Africans.
Baada ya kusikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili Kamati imeona kuwa shauri hilo la mapitio (Review) halina msingi wa kisheria kushawishi Kamati kubadili maamuzi yake yaliyotolewa awali na hivyo imetupilia mbali shauri hilo.
TFF imesema kuwa sababu kwa undani za uamuzi huo zitatolewa kwa pande zote mbili zinazohusika katika shauri hilo Jumatatu ya tarehe 6 Machi, 2023.
Baada ya shauri hilo kutupiliwa mbali Feisal Salum Abdallah atakuwa na nafasi ya kwenda kwenda Mamlaka za juu zaidi ambako ni CAS, endapo hajaridhika na maamuzi hayo.
Kwa sasa Feisal anabaki kuwa Mchezaji halali wa Young Africans.
- MSIMAMO Kundi D CAF Confederation Cup 2022-2023
- MSIMAMO Kundi C CAF Champions League 2022-2023
- Namna ya Kujisajili na Premier Bet Ushinde Mamilioni
- RATIBA kamili ya hatua ya 16 Bora Azam Sports Federation Cup 2023
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
- RATIBA ya Yanga CAF Confederation Cup 2022/2023 hatua ya Makundi
- RATIBA ya Simba CAF Champions League hatua ya Makundi
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.
DONWLOAD NIJUZE TV HAPA SISI kwetu Michezo ndiyo Furaha YETU.
The post TFF yatupilia mbali shauri la Feisal (maombi yake hayana mashiko) appeared first on Nijuze Mpya.
from Michezo – Nijuze Mpya https://ift.tt/gPUjR7f
via IFTTT
No comments:
Post a Comment