Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Chelsea wanataka kitita cha pauni milioni 70 kumuuza kiungo wa kati wa England Mason Mount, 24, licha ya kusalia na mwaka mmoja wa mwisho wa kandarasi yake. (Athletic)
Mount ana nia ya kujiunga na Bayern Munich na kuungana na meneja wake wa zamani wa Chelsea Thomas Tuchel. (Guardian)
Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wanakaribia kukamilisha dili la kocha msaidizi wa Chelsea Muingereza Anthony Barry. (90Min)
Lakini kiungo wa kati wa West Ham Declan Rice, 24, hasakwi na Bayern na hawakufanya mkutano na wawakilishi wa mchezaji huyo wa kimataifa wa England wiki iliyopita. (Sky Sports Ujerumani)
Klabu ya Saudi Arabia Al Hilal inataka kumfanya mshambuliaji wa Paris St-Germain na Argentina Lionel Messi, 35, kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani. (Mirror)
Lakini klabu ya Ligi Kuu ya Soka ya Inter Miami ina matumaini ya kumsajili Messi na kiungo wa kati wa Barcelona na Hispania Sergio Busquets, 34, msimu ujao. (Sport)
Mshambulizi wa Tottenham na England Harry Kane, 29, anasakwa na Manchester United wanaosaka mshambuliaji, hata hivyo mshambuliaji wa Ajax Mghana Mohammed Kudus, 22, na mchezaji wa kimataifa wa Ureno wa Benfica Goncalo Ramos, 21, ni miongoni mwa chaguzi zao nyingine. (Manchester Evening News)
Matumaini ya Manchester United ya kumsajili kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong, 25, yameongezeka kufuatia Barcelona kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Manchester City na Ujerumani Ilkay Gundogan, 32. (Mirror)
Wakala wa Gundogan amekanusha kuwa nahodha huyo wa Manchester City ameshafanya maamuzi kuhusu mustakabali wake, ingawa yuko tayari kuhama. (Guardian)
West Ham huenda ikaachana na meneja wao David Moyes mwishoni mwa msimu huu, bila kujali kama klabu hiyo itaepuka kushushwa daraja. (90Min)
Leeds United inaweza kumgeukia meneja wa zamani wa Crystal Palace, Mfaransa Patrick Vieira, katika majira ya joto, ikiwa bosi wa Uhispania Javi Gracia - aliyeteuliwa kama mrithi wa Jesse Marsch hadi mwisho wa msimu - ataondoka. (TalkSPORT)
Beki wa Manchester City na Uhispania Aymeric Laporte, 28, analengwa na Paris St-Germain. (Football Insider)
Chelsea na Tottenham wako tayari kupigana kumsajili beki wa Inter Milan na Italia Alessandro Bastoni, 23, msimu huu wa joto. (Fichajes - kwa Kihispania) Mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 36, anatazamiwa kusaini mkataba mpya na AC Milan ambao utaendelea hadi 2024. (Fabrizio Romano)
AC Milan wamepewa ofa ya kiungo wa kati wa Guinea Naby Keita, 28, kabla ya kuondoka Liverpool msimu huu mkataba wake utakapomalizika. (Calciomo)
Jose Mourinho ameiambia Roma kuwa anataka kuheshimu kandarasi yake, ambayo itaendelea hadi 2024. Kumekuwa na uvumi kwamba bosi huyo wa Ureno anataka kuihama klabu hiyo huku akihusudiwa na Paris St-Germain. (Corriere dello Sport)
BBC
No comments:
Post a Comment