Tetesi za usajili barani ulaya Leo Jumanne March 28 - EDUSPORTSTZ

Latest

Tetesi za usajili barani ulaya Leo Jumanne March 28

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 
Manchester City haina mpango wa kumuuza kiungo wake wa kati wa Muingereza Kalvin Phillips msimu huu wa joto, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kucheza mechi chache tu tangu kuhamia Ettihad kutoka Leeds United. (Football Insider)


Hata hivyo, Phillips anasemekana kuwa atakua tayari kuondoka City huku kukiwa na hofu kwamba kukosa muda mwingi wa kucheza kunaweza kuathiri nafasi yake ya kuchaguliwa kwenye kikosi cha England. (90min)


Mshambuliaji wa Paris St-Germain na Argentina Lionel Messi, 35, anaweza kuhamia MLS msimu huu wa joto - huku kila klabu kati ya 29 kwenye ligi ikichangia mshahara wake. (Sport)


PSG wanaendelea kuwasiliana na wawakilishi wa kiungo wa kati wa Chelsea na Ufaransa N'Golo Kante, 31 kwa ajili ya mkataba mpya (90min).


Mshambuliaji wa Leeds United Rodrigo, 32, huenda alazimika kupunguzwa mshahara ikiwa atatia saini kandarasi mpya katika klabu hiyo. Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania unatarajiwa kumalizika msimu wa joto wa 2024. (Football Insider)


Mshambuliaji wa England Bukayo Saka, 21, atapokea takriban £15m kwa msimu atakapotia saini mkataba wake mpya na Arsenal. (Mail)


Liverpool bado hawajaanza mazungumzo ya kandarasi na kiungo wa zamani wa England James Milner licha ya Jurgen Klopp kutaka kumbakisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 kwa mwaka mwingine. (Athletic)


Chelsea italazimika kuongeza kiasi kikubwa cha pesa kwa kuwauza wachezaji msimu huu ili kuepuka kukiuka kanuni za kifedha za Ligi Kuu ya Uingereza mwaka ujao. (Hour - usajili unahitajika)


Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy anataka kujua kama Julian Nagelsmann yuko tayari kuchukua nafasi ya Antonio Conte kama kocha mkuu wa Spurs. (Mail)


Kikosi cha Bayern Munich kimegawanyika katika makundi mawili kuhusu uamuzi wa kumfuta kazi meneja wa Ujerumani Julian Nagelsmann, 35. (Bild, via Goal)


Tottenham ni miongoni mwa klabu kadhaa za Ligi kuu England zinazomtaka mshambuliaji wa Brighton na Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson, 18. (Football Insider)


Borussia Dortmund wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Ireland Kaskazini mwenye umri wa miaka 19 Shea Charles kutoka Manchester City. (Bild)


Barcelona italazimika kusajili angalau wachezaji watatu hadi wanne kwa uhamisho wa bure msimu huu wa joto na kufanya kazi ndani ya bajeti ndogo ya mishahara. (Mundo Deportivo)


BBCDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz