TANZIA: Iddy Mobby Afariki Dunia
Beki wa Mtibwa Sugar, Iddy Moby Mfaume amefariki Dunia leo Machi 5 mchana katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, Jijini Dodoma.
Daktari wa Hospitali ya Kampuni ya Mtibwa Sugar, Khalid Sabuni, amesema kuwa Mobby alipata tatizo la kiafya jana (Machi 4, 2023) mkoani Morogoro wakati akiwa katika mazoezi binafsi ya kutembea (road walk) kuelekea mchezo wao wa Azam Sports Federation Cup dhidi ya KMC.
“akiwa anaelekea uwanjani, alianza kupata tatizo la kuumwa kichwa, kisha alisikia kizunguzungu na kutaka kuanguka lakini alipiga magoti”, amesema Dkt. Sabuni wakati akithibitisha kifo chake.
Dkt. Sabuni amesema kuwa baada ya tukio hilo Mobby alipelekwa katika hospitali ya Kampuni hiyo, na kisha hospitali ya Bwagala kwaajili ya matibabu zaidi lakini ilipofika usiku hali ilikuwa mbaya na hivyo kupewa rufaa kwenda Hospitali ya Benjamin Mkapa, Jijini Dodoma ambako umauti umemfika.
“alifika Dodoma usiku lakini kufikia mchana wa leo akawa amefariki”, amehitimisha Dkt. Sabuni.
Iddy Mobby alisajiliwa Mtibwa Sugar msimu huu akitokea Ruvu Shooting lakini aliwahi pia kuzichezea timu za Geita Gold FC ya Geita, Polisi Tanzania, na Mwadui FC kwa nyakati tofauti na pia aliwahi kuitwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
Uongozi wa Nijuze Habari unatoa pole kwa ndugu, jamaa na Wapenzi wa Soka ulimwenguni kote kwa kuondokewa na ndugu yetu Iddy Mobby.
- MSIMAMO Kundi D CAF Confederation Cup 2022-2023
- MSIMAMO Kundi C CAF Champions League 2022-2023
- Namna ya Kujisajili na Premier Bet Ushinde Mamilioni
- RATIBA kamili ya hatua ya 16 Bora Azam Sports Federation Cup 2023
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
- RATIBA ya Yanga CAF Confederation Cup 2022/2023 hatua ya Makundi
- RATIBA ya Simba CAF Champions League hatua ya Makundi
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.
The post TANZIA: Iddy Mobby Afariki Dunia appeared first on Nijuze Mpya.
from Michezo – Nijuze Mpya https://ift.tt/am0VhMd
via IFTTT
No comments:
Post a Comment