Taarifa Mpya na Njema Kwa wanayanga kuhusu Morrison - EDUSPORTSTZ

Latest

Taarifa Mpya na Njema Kwa wanayanga kuhusu Morrison

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 

Winga mtukutu wa Yanga Bernard Morrison yuko tayari kurejea kikosini baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa takribani miezi mitatu


Mara ya mwisho Morrison kuonekana uwanjani akiitumikia Yanga ulikuwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Disemba 23 na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-2


Morrison alishiriki kikamilifu katika kupatikana kwa ushindi huo akitengeneza bao la kusawazisha lililofungwa na Fiston Mayele


Kiuhalisia Morrison ana deni kubwa kwa uongozi na mashabiki wa Yanga ambao walikuwa na imani kubwa katika urejeo wake


Pamoja na usumbufu aliowasababishia Wananchi pale alipotoroka nyumbani, lakini aliporejea walimpokea kwa mikono miwili


Baada ya kupona majeraha, wengi wanatarajia Morrison ataifanya vyema kazi iliyomrejesha Yanga


Majeraha yalipelekea asiwe na mchango katika mapambano ya kuipeleka Yanga robo fainali ya michuano ya Shirikisho (CAF), anaweza kuwa na mchango kule DR Congo kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe ambao Yanga inahitaji kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kumaliza kinara wa kundi


Aidha bado kuna mechi sita za kuhitimisha msimu ambazo anaweza kushiriki pamoja na mechi za kombe la FA Yanga ikiwa hatua ya robo fainaliDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz