Simba yaifumua HOROYA Ac 7-0 huyu chama Mhhhh!! - EDUSPORTSTZ

Latest

Simba yaifumua HOROYA Ac 7-0 huyu chama Mhhhh!!

Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA

Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Simba inakwenda robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika kibabe kabisa kwa ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Horoya Ac katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa


Hizi ni salamu kwa vigogo wote Afrika kuwa Simba iko tayari kushindania ubingwa msimu huu


Mnyama alianza kampeni yake taratibu kwa kupoteza mechi mbili za kwanza lakini leo anakwenda robo fainali kwa ushindi mkubwa zaidi katika michuano hiyo msimu huu


Ilikuwa siku nzuri kwa Clatous Chama 'Mwamba wa Lusaka' ambaye leo ameondoka na mpira akifunga mabao matatu


Sadio Kanoute leo amewaonyesha kuwa yeye sio kukata umeme tu, hata kufunga anaweza, akiweka kambani mabao mawili yote akimtungua mlinda lango kutoka nje ya 18


Jean Baleke katika ubora mkubwa kabisa akaweka kambani mabao mawili pia sasa akifunga mabao matano katika mechi mbili


Ilikuwa mechi ya upande mmoja, Simba walitawala na pengine Horoya Ac wangeondoka na nyingi zaidi


Kwa hakika Simba sasa iko tayari kutimiza malengo yake ya angalau kucheza nusu fainali ya michuano hiyo msimu huu



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz