Nabi awataja wachezaji watakao kosekana kesho kwenye mechi Yao dhidi ya Monastri - EDUSPORTSTZ

Latest

Nabi awataja wachezaji watakao kosekana kesho kwenye mechi Yao dhidi ya Monastri

Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA

Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amewataka mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa kesho katika mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya US Monastir


Nabi amewataka mashabiki waujaze uwanja wa Benjamin Mkapa ili kuwapa nguvu wachezaji wao kuhakikisha wanapambana kuibuka na ushindi katika mchezo ambao wanatarajia kuwa mgumu


"Nawaomba mashabiki wa Yanga waje kwa wingi uwanjani. Tunataka muwe sambamba nasi, mtushangilie katika nyakati zote. Wachezaji wetu watapambana sana pale mtakapokuwa mnawashangilia kuliko mkiwa kimya"


"Monastir ni timu nzuri hawakuja hapa kutembea najua wamekuja kutafuta matokeo mazuri ili wajihakikishie kuwa vinara wa kundi. Nawapongeza kwa kufikisha miaka 100 siku ya jana, najua kesho watakuja kupambana ili wafanye maadhimisho yao vyema"


"Sisi tumejiandaa kwa ajili ya mchezo huo na lengo letu ni kutafuta ushindi ili tuweze kufuzu robo fainali," alisema Nabi


Akizungumzia hali ya kikosi, Nabi amesema wachezaji David Bryson, Benard Morrison na Denis Nkane watakosekana katika mchezo huo


Bryson ni majeruhi wakati Morrison na Nkane wameanza mazoezi mapesi lakini hawako tayari kwa mchezo huo


Nabi alibainisha kuwa wachezaji Fiston Mayele na Kennedy Musonda walikuwa na majeraha madogo lakini wako tayari kwa mchezo huo



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz