"Nitahakikisha tunakuwa na kikosi Bora" Robertinho - EDUSPORTSTZ

Latest

"Nitahakikisha tunakuwa na kikosi Bora" Robertinho

 

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA

Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA

Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

SIMBA inaendelea kupiga hesabu za kucheza hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini kocha wa timu hiyo Roberto Oliveira ‘Robertinho’ akili yake iko mbali sana - kuna kazi moja ya kibabe anaifanya itakayowashtua na kuwafurahisha mashabiki wa timu hiyo.

Robertinho anachofanya kwa sasa kwa kila mchezo anaocheza uwe wa kimataifa au wa ndani anakuwa na kazi nyingine ya kufikiria usajili wa msimu ujao akiwasoma mastaa bora anaokutana nao katika mechi kisha kubaki na faili lao ili usajili ukianza awe amemaliza kila kitu.

Robertinho ameliambia Mwanaspoti kuwa tayari ana majina makubwa ya wachezaji wa nje na ndani katika faili lake na hao sio kwamba amemaliza pia anawafuatilia taratibu katika mechi zingine juu ya mwendelezo wa ubora.

Simba imetinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa ikiwa nafasi ya pili ya Kundi C ikiwa na pointi tisa nyuma ya vinara Raja Casablanca watakaomaliza nao mechi ya mwisho wenye pointi 13, lakini kocha huyo raia wa Brazili amesema anataka kufanya kazi hiyo mapema kisha atakaa na mabosi wa timu kufanya uamuzi wa mwisho lengo likiwa wawe na kikosi bora kitakachokusanya mataji.


Simba iliyotinga robo fainali kwa sasa ina mastaa walioibeba hatua hiyo akiwamo Clalous Chama mwenye mabao manne akiwa kinara wa ufungaji wa ligi hiyo ya mabingwa, Moses Phiri mabao matano kwenye mechi za awali, Jean Baleke, Saido Ntibazonkiza, Hennock Inonga, Sadio Kanoute na Pape Ousmane Sakho aliyetwaa tuzo ya Bao Bora la Kombe la Shirikisho msimu uliopita.

“Kwenye kila mchezo kazi yangu haishii tu kuhakikisha tunashinda, lakini tunatafuta watu bora ambao tunawaona na baada ya hapo nawafuatilia baadaye je viwango vyao bora vimeendelea au aliocheza kwa ubora tulipokutana naye tu,” alisema Robertnho.

“Tunafuatilia wachezaji wote wa ndani na wa nje kuangalia wapi tunataka kuongeza mtu kulingana na ubora tunaouona kwa wachezaji tulionao sasa na baadaye nitakaa na viongozi mapema kufanya maamuzi.”


Aidha Robertinho aliongeza kwa kikosi chake cha msimu ujao anataka kiwe na uwiano mzuri kwa kila nafasi kuwa na wachezaji wawili wenye ubora wa juu na unaokaribiana ili kutengeneza ushindani mzuri.

“Ukiangalia sasa kuna nafasi kuna wachezaji zaidi ya wawili, nadhani namna nzuri ni kuwa na uwiano mzuri wa wa kikosi, tunaweza kuwa na kikosi cha wachezaji ambao kila nafasi kuna watu wawili lakini kitu muhimu hapa ubora wao uwe mkubwa hata ukilingana sio mbaya na baadaye tuwaache washindanie nafasi.

“Nitahakikisha tunakuwa na kikosi bora sana kwa kuwa mashindano tunayoshiriki na ubora wa timu pinzani yanatulazimisha kuwa na ubora huo lakini hapa lazima tukubaliane Simba ina jina kubwa na lazima mchezaji tutakayekuwa naye awe na hadhi ya jina la Simba nafikiri hili ni kubwa.

“Simba inashiriki mashindano makubwa dhidi ya klabu zingine kubwa za ndani na nje ya nchi lazima mchezaji atambue kwamba anapokuja Simba awe na utayari wa kuipigania klabu hii kubwa na sio kuja kusota benchi na kushindwa kupigania nafasi.”


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz