Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Winga machachari wa Yanga Jesus Moloko amewataka mashabiki kuchangamkia fursa ya kusafiri na timu DR Congo kwa ajili ya mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe
Mchezo huo utapigwa April 02 katika dimba la TP Mazembe jiji la Lubumbashi, Yanga kihitaji kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kumaliza kinara wa kundi D
Moloko amesema wachezaji wangependa kuona lile 'vibe' la mashabiki katika dimba la Mkapa likihamia Lubumbashi
"Ujumbe wangu kwa mashabiki wa Yanga waje kwa wingi twende Congo. Sisi wachezaji tuko tayari na tunawaahidi tutakwenda kupambana kuhakikisha tunapata ushindi," alisema Moloko
Kwa Moloko haitakuwa mara yake ya kwanza kucheza kunako dimba la TP Mazembe kwani kabla ya kutua Yanga aliitumikia AS Vita
Yanga itasafiri DR Congo ikiwa na faida ya wachezaji sita ambao waliwahi kuitumikia AS Vita
Tuisila Kisinda, Fiston Mayele, Djuma Shaban, Joyce Lomalisa na Yannick Bangala hawatakuwa wageni katika uwanja wa TP Mazembe
No comments:
Post a Comment