Mayele, Kaze wafunguka haya kuelekea mechi yao dhidi ya Geita gold kesho - EDUSPORTSTZ

Latest

Mayele, Kaze wafunguka haya kuelekea mechi yao dhidi ya Geita gold kesho


Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema kikosi kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Geita Gold ambao utapigwa kesho Jumapili March 12 katika uwanja wa Azam Complex


Kaze amesema wanatambua mechi dhidi ya Geita Gold haijawahi rahisi lakini wamejipanga kushinda mchezo huo ili kuwa kwenye nafasi nzuri ya kutetea ubingwa kwa msimu wa pili mfululizo


"Tunakwenda kucheza mechi ngumu dhidi ya Geita Gold, timu yenye Mwalimu mwenye uzoefu mkubwa na ligi ya Tanzania. Mechi hii haijawahi kuwa rahisi lakini tunapaswa kupambana ili kupata ushindi"


"Tumetoka kucheza mechi ngumu ya Shirikisho dhidi ya Real Bamako, tuna changamoto ya uchovu na fatique lakini tunapaswa kufanya nguvu zote ili kuhakikisha tunashinda na kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wetu," alisema Kaze


Nae mshambuliaji kinara wa mabao ligi kuu ya NBC, FIston Mayele amesema wachezaji watapambana ili kuhakikisha wanatimiza malengo ya kutwaa ubingwa


Mayele amesema yeye binafsi anatamani kuibuka mfungaji bora msimu huu hivyo ataendelea kupambana kwa kushirikiana na wachezaji wenzake kwanza kutimiza malengo ya timu na yake


Mayele ameishukuru klabu ya Yanga kwa kumsaidia kupata nafasi ya kuitwa timu ya Taifa ya DR Congo akiwapa shukrani wadau na mashabiki wa soka nchini ambao wanamuunga mkono


Je unatafuta Ajira tembelea tovuti hii Sasa Kwa matangazo yote ya kazi BOFYA HAPA SASA



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz