Matokeo Mtibwa sugar vs Simba leo Jumamosi February 11,2023 - EDUSPORTSTZ

Latest

Matokeo Mtibwa sugar vs Simba leo Jumamosi February 11,2023


Mnyama Simba ameunguruma dimba la Manungu Complex huko Turiani mkoani Morogoro wakiibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu ya NBC


Simba ilihitaji dakika 45 tu kujihakikishia ushindi huku ikihitaji dakika saba tu kufunga mabao mawili ya haraka kupitia kwa Jean Baleke ambaye leo alikuwa shujaa wa Simba baada ya kufunga hat-trik


Akiwa katika kiwango bora, Baleke aliwaweka kwenye wakati mgumu walinzi wa Mtibwa Sugar akiongeza bao la tatu kwenye dakika ya 36 akimalizia mpira wa kichwa kutoka kwa Shomari Kapombe

Kuziona Yanga vs Geita gold kesho ni buku mbili tu

Baleke amedhihirisha Simba haikufanya makosa kwenda kumsajili kule TP Mazembe. Ametua mwezi Januari na tayari amepachika mabao matano kwenye ligi


Ni ushindi muhimu kwa Simba ambao umewafanya wafikishe alama 57 sasa wakiwa nyuma ya Yanga kwa tofauti ya alama tano


Yanga watacheza na Geita Gold hapo kesho kwenye mchezo utakaopigwa uwanja wa Azam Complex

Je unatafuta Ajira tembelea tovuti hii Sasa Kwa matangazo yote ya kazi BOFYA HAPA SASA



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz