Kocha wa timu ya taifa Taifa Stars, Adel Mrouche amepewa nafasi ya kuchagua wataalamu 4 atakaoambatana nao kwenye timu ya taifa kama sehemu ya benchi lake la ufundi, Kocha huyo amependekeza jina la kocha msaidizi wa klabu ya Yanga, Cedric Kaze kuwa chaguo lake la kwanza.
Ikumbukwe Cedric Kaze alifundishwa na kocha Adel Mrouche. Mrouche ni mkufunzi wa shirikisho la soka Ulaya UEFA kwenye kozi ya UEFA pro license.
Tayari klabu ya Yanga imeshapokea ombi hilo kutoka TFF, kinachosubiriwa kwa sasa ni maamuzi ya muhusika. Klabu imempa baraka zote Cedric Kaze iwapo ataamua kujiunga na timu ya taifa.
No comments:
Post a Comment