Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Droo ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya imefanyika leo ambapo mabingwa wa Uingereza Manchester City watakuwa na shughuli pevu mbele ya Bayern Munich katika mtanange wa robo fainali
Itakuwa mechi ya kwanza ya mashindano kwa Pep Guardiola kuchuana na waajiri wake wa zamani, Bayern Munich
Mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo, Real Madrid wao watachuana na Chelsea
Ni droo ambayo mpaka nusu fainali itabakisha timu moja tu kati ya vigogo Real Madrid, Man City na Bayern kwani mshindi wa mchezo kati ya Man City dhidi ya Bayern Munich kwenye nusu fainali atakumbana na mshindi wa mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya Chelsea
Ac Milan itachuana na Napoli katika mchezo mwingine wakati Benfica ikichuana na Inter Milan
Washindi wa mechi hizo juu watakutana kwenye nusu fainali.
No comments:
Post a Comment