Jinsi Kocha Nabi alivyofanikisha kuwaunganisha Musonda na Mayele - EDUSPORTSTZ

Latest

Jinsi Kocha Nabi alivyofanikisha kuwaunganisha Musonda na Mayele


 Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA

Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Wakati Kennedy Musonda anatua Yanga dirisha dogo, wengi walijiuliza ni kwa namna gani Kocha Nasreddine Nabi ataweza kumtumia sambamba na mshambuliaji wake namba moja Fiston Mayele


Musonda aliondoka Power Dynomos kuijunga na Yanga akiwa kinara wa mabao huko Zambia akifunga mabao 11


Mifumo yote anayopenda kutumia Nabi ni kuweka mshambuliaji mmoja mbele. Changamoto ilionekana katika mechi za mwanzo.


Lakini sasa Nabi amepata mfumo sahihi wa kuwatumia Musonda na Mayele na unaweza kusema pacha yao imewaka!


Nabi anamtumia Musonda kama wingi anayetokea upande wa kushoto lakini mara nyingi huingia ndani kuungana na Mayele wakati Joyce Lomalisa akipanda


Tayari Musonda amefunga mabao matano katika mashindano yote, mabao mawili amefunga kombe la FA, bao moja amefunga kwenye ligi na mabao mawili amefunga kwenye kombe la Shirikisho


Katika michuano ya kombe la Shirikisho Musonda ndio kinara wa kutengeneza mabao akiwa na assist tatu, mbili akiwa amemtengenezea Mayele


Mayele ndiye kinara wa mabao kombe la Shirikisho akiwa ameweka kambani mabao matatuDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz