Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Chama alifunga hat-trik katika mchezo dhidi ya Horoya Ac uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa March 18 na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 7-0
Pia alifunga bao pekee la ushindi kwenye mchezo dhidi ya Vipers Fc uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa March 07
Katika hatua ya makundi Chama amepachika mabao manne na kutoa assist moja akiwa sawa na mshambuliaji Al Hilal Makabi Lilepo ambaye pia amefunga mabao manne na assit moja
Wachezaji wanaofuatia ambao wamefunga mabao matatu ni Hamza Khabba wa Raja Casablanca ya Morocco, Mahmoud Kahraba wa Al Ahly ya Misri, Cassius Mailula na Peter Shalulile wote wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ambao kila mmoja ametupia mara tatu.
Chama alikuwa mchezaji bora wa wiki wa michuano hiyo baada ya mechi za raundi ya nne na ana nafasi kubwa ya kushinda tuzo hiyo baada ya mechi za raundi ya tano
Post a Comment