Wakiwa wamewasili salama mkoani Morogoro, Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliviera ‘Robertinho’, amesema anatarajia kutumia mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar itakayochezwa kesho kama sehemu ya maandalizi ya kuwakabili Horoya AC kutoka Guinea
Simba itaikaribisha Horoya AC katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayochezwa Machi 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Robertinho amesema kikosi chake kiko imara na tayari kuzisaka pointi tatu dhidi ya Mtibwa Sugar ili kuendelea kujiweka katika sehemu salama kwenye mbio zao za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kocha huyo alisema anafahamu Mtibwa Sugar ni moja ya timu nzuri hapa nchini, hivyo watacheza kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha wanaendelea kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi hiyo.
"Kupata pointi tatu kutoka kwa Mtibwa Sugar kutatupa morali kuelekea mechi ijayo ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya AC. Tunataka kuendelea kupata matokeo bora, itatusaidia kujiamini zaidi," alisema kocha huyo
Aliongeza mechi hiyo dhidi ya Mtibwa Sugar itakuwa na ushindani kwa sababu wenyeji wanahitaji kulinda heshima ya kucheza nyumbani na wao wanahitaji kuondoka na pointi tatu muhimu.
"Tunaifahamu Mtibwa Sugar, tunajua haitakuwa mechi rahisi kutokana na ubora walionao hasa kwa sababu watakuwa wanacheza kwenye Uwanja wa nyumbani, tunahitaji matokeo chanya katika mchezo wetu wa Jumamosi"
"Hii mechi itakuwa na mambo mawili, kuhitaji ushindi na kurejea nyumbani na pointi tatu, lakini inawapa wachezaji wangu molari kuelekea mechi yetu ijayo ya kimataifa,” alisema Kocha huyo"
Katika mechi ya kesho, Simba itawakosa nyota wake wanne ambao ni Kibu Denis, Ismael Sawadogo na Augustine Okrah ambao ni majeruhi na kipa chaguo la pili, Beno Kakolanya, ambaye ana ruhusa maalum kwa ajili ya kumaliza matatizo yake ya kifamilia.
Je unatafuta Ajira tembelea tovuti hii Sasa Kwa matangazo yote ya kazi BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment