Baada ya ushindi wa mabao 3-0 tuliopata dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Manungu Complex kikosi kimeanza safari ya kurejea jijini Dar es Salaam.
Baada ya timu kufika wachezaji watapewa mapumziko ya siku moja ambapo watarejea mazoezini Jumatatu kuanza maandalizi ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya FC kutoka Guinea.
Matokeo Mtibwa sugar vs Simba leo
Mchezo dhidi ya Horoya utapigwa Jumamosi Machi 18, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.
Ushindi katika mchezo huo ndio utatupa tiketi ya kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ndio maana tunaupa umuhimu mkubwa.
Je unatafuta Ajira tembelea tovuti hii Sasa Kwa matangazo yote ya kazi BOFYA HAPA SASA
No comments:
Post a Comment