Feisal bado hajaripoti kambini ~ Alikamwe - EDUSPORTSTZ

Latest

Feisal bado hajaripoti kambini ~ Alikamwe

 


Imeelezwa kuwa mchezaji wa Yanga, Feisal Salum hajaripoti klabuni hapo kama alivyotakiwa kufanya na timu hiyo.

Ifahamike baada ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka TFF kutupilia mbali shauri la marejeo la mchezaji huyo, Yanga ilitoa taarifa Machi 6, 2023 ya kumtaka Feisal aripoti kambini kama mchezaji wao halali.

Feisal kukutana na mabosi wa Yanga muda wowote

Akizungumza na waandishi wa waandishi wa habari Afisa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe amelazimika kutoa taarifa hiyo baada ya shabiki mmoja wa Yanga kupiga simu na kutaka kujua endapo Feisal amerejea klabuni.

Akitoa majibu ya swali hilo Kamwe amejibu kwa ufupi kwa kusema “hajaripoti”

Je unatafuta Ajira tembelea tovuti hii Sasa Kwa matangazo yote ya kazi BOFYA HAPA SASADownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz