Gianni Infantino achaguliwa Tena kuliongoza shirikisho la kandanda Duniani "FIFA" - EDUSPORTSTZ

Latest

Gianni Infantino achaguliwa Tena kuliongoza shirikisho la kandanda Duniani "FIFA"

Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA

Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
 
Rais wa shirikisho la kandanda Duniani Gianni Infantino amesema kwamba ataendelea kuimarisha kukua kwa sekta ya soka ulimwenguni kwa kuinua kiwango cha mpira wa watoto wadogo.

Infantino ameyasema hayo mjini Kigali Rwanda baada ya kuchaguliwa kuongoza tena kwa kipindi cha miaka minne ijayo hapo Jana Alhamisi ya Machi 16,2023.

Gianni Infantino alichaguliwa kwa wingi wa kura za wajumbe wote 208 waliohudhuria kongamano la 73 la FIFA lililofanyika Kigali kati ya nchi 2011 wanachama wa FIFA.

Kongamano la FIFA Mjini Kigali lilianza mapema wiki hii ambapo zilifanyika shughuli kadhaa ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa uwanja wa mpira wa Kigali uliopewa jina la Pele nyota wa Brazil aliyengáa kwenye medani za soka ulimwenguni’

Mara baada ya kuchaguliwa tena Gianni Infantino amesema atazidisha ushirikiano wa mataifa wanachama.

“Nawahakikishia kuendeleza ushirikiano wa pamoja nanyi,, napenda niwakumbushe kwamba michezo ni starehe, furaha, mapenzi na amani. Jambo jingine napenda niseme kwamba michezo ili iunge dunia yetu iweze kuwa nzuri zaidi’’alisema.

“Ni heshima na upendeleo wa ajabu, na jukumu kubwa,” Infantino alisema.

“Ninaahidi kuendelea kutumikia FIFA na soka Duniani kote.

“Kwa wale wanaonipenda, na najua kuna wengi, na wale wanaonichukia … nawapenda ninyi nyote.”

Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema kwamba wakati ambapo Dunia inatawaliwa na siasa za chuki na undumilakuwili soka ni kiunganishi muhimu.

Amesema kwamba mataifa yanapaswa kushirikiana ili kukomesha tabia mbaya ya ubaguzi

“Mashabiki wanapowarushia ndizi mbivu wachezaji wa kiafrika, hii ni kwa sababu ya mazingira mabovu ya kijamii ambayo yanasababisha tabia hizo mbovu.

Kwa hiyo tunatakiwa kushirikiana kuhakikisha kwamba michezo inakuwa jumuishi na ya kuheshimiana” alisema Kagame.

Naye nyota wa zamani wa Nigeria Jay Jay Okocha amesema maandalizi ya kongamano la 73 la FIFA na mafanikio yake ni ishara kwamba sasa Afrika inaanza kujizatiti zaidi

“Hili ni jambo sisi sote kama waafrika tunapaswa kulichukulia kama letu na ni ishara kwamba kumbe tukiweka nguvu zetu pamoja tunaweza kufanikiwa” alisema Okocha.

Kwenye kongamano hilo Gianni Infantino mwenye umri wa miaka 52 amesifiwa kutokana na mafanikio yake katika kuleta mabadiliko katika ufanisi wa maendeleo ya vyama vya mpira katika mataifa wanachama wa FIFA.

Ruzuku ya pesa kwa vyama vya mpira ilipanda kutoka dola laki mbili na nusu hadi milioni mbili ndani ya kipindi cha miaka saba iliyopita.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz