Burkinafaso yafuzu Afcon - EDUSPORTSTZ

Latest

Burkinafaso yafuzu Afcon

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 
Wakati Tanzania tukilazimika kusubiri hatma yetu katika mechi mbili za mwisho kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2023, Stephane Aziz Ki akiwa na timu ya Taifa ya Burkina Faso, wamefuzu kwa michuano hiyo itakayofanyika Ivory Coast mwezi Januari 2024

Licha ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Togo jana, Burkina Faso wamefuzu wakiwa vinara wa kundi B baada ya kufikisha alama 10

Mali anayocheza mlinda lango Djigui Diarra jana ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Gambia, bado inaongoza kundi  G ikiwa na alama 9

Fiston Mayele na DR Congo wakalazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Mauritania wakati juzi Zambia wanayocheza Kennedy Musonda na Lazarus Kambole walipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Lesotho na kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu baada ya kufikisha alama 9

Nyota wote wa Yanga tayari wamekamilisha majukumu yao katika timu za Taifa ambapo baadhi ya wachezaji wanatarajiwa kujiunga na wenzao Avic Town leo tayari kwa safari ya DR Congo kesho AlhamisiDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz