Ally Kamwe azidi kutamba tu ni kuhusu hili - EDUSPORTSTZ

Latest

Ally Kamwe azidi kutamba tu ni kuhusu hili


Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Wakiwa tayari wamejihakikishia kucheza robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika, Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema wako tayari kucheza na yeyote kwenye hatua ya robo fainali


Yanga inaongoza kundi D ikiwa na alama 10 sawa na US Monastir lakini Wananchi wana uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa


Mabingwa hao wa Tanzania Bara watasafiri kwenda Lubumbashi siku ya Alhamisi, March 30 kukamilisha mechi ya mwisho hatua ya makundi dhidi ya TP Mazembe


Kamwe amesema mkakati wa Yanga ni kushinda mchezo huo ili kuhakikisha wanamaliza vinara wa kundi na kuwa na uhakika wa kumaliza mechi ya pili ya robo fainali katika uwanja wa Benjamin Mkapa


Kamwe amesema kiwango bora walichoonyesha katika michuano hiyo msimu huu kimeifanya Yanga kuwa moja ya timu zinazohofiwa


"Ukifuatilia tangu ligi ya mabingwa, tulipoteza mchezo mmoja dhidi ya Al Hilal kule Sudan. Kwenye kombe la Shirikisho pia tukapoteza mchezo mmoja kule Tunisia dhidi ya US Monastrir lakini tukalipa kisasi hapa nyumbani"


"Msimu huu sisi ndio timu pekee iliyoshinda mechi zote tatu kwenye michuano ya CAF hatua ya makundi katika uwanja wa Benjamin Mkapa huku tukifunga zaidi ya bao moja katika kila mchezo. Ushindi wetu dhidi ya US Monastir naamini umetoa somo kwa wengine kujifunza jinsi ya kuzifunga timu za waarabu"


"Kwa hatua ambayo tumeifikia sasa, hatuihofii timu yoyote bali sisi ndio tunahofiwa. Tuna kikosi bora na benchi bora la ufundi linaoongozwa na profesa Nasreddine Nabi," alitamba KamweDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz