Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mtananange huo wa dabi ya Afrika Mashariki, utapigwa kuanzia saa 2 usiku
Huu ni mchezo muhimu kwa Tanzania kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu michuano ya Afcon 2023 ambayo itafanyika baadae mwaka huu huko Ivory coast
Ushindi kwa Stars dhidi ya Uganda leo utawafanya wafikishe alama saba hivyo kuhitaji alama moja tu katika mechi mbili zitakazokuwa zimebaki dhidi ya Niger na Algeria ili kufuzu
Jana Niger ilichapwa bao 1-0 na Algeria na hivyo kuwahakikisha Algeria kuwa timu ya kwanza kufuzu kwa michuano hiyo baada ya kufikisha alama tisa
Tanzania inashika nafasi ya pili ikiwa na alama nne, Niger ni wa tatu wakiwa na alama mbili wakati Uganda wanaburuza mkia wakiwa na alama moja katika kundi F
Stars inahitaji angalau alama nane tu kuweza kufuzu, alama tatu lazima zipatikane kwa Mkapa leo halafu kumaliza kazi hapohapo kwa Mkapa kwenye mchezo utakaofuata dhidi ya Niger mwezi Juni
Habari njema ni kuwa hakuna kiingilio kwa majukwaa ya Mzunguuko, mageti ya dimba la Mkapa yatafunguliwa kuanzia saa sita mchana
Kuwahi kwako uwanjani ndio tiketi yako kwani uwanja utakapokuwa umejaa, mageti yatafungwa!
No comments:
Post a Comment