Ally Kamwe awatupia dongo hili watani zao Simba hii ni baada ya kushinda mechi ya Jana dhidi ya Monastri - EDUSPORTSTZ

Latest

Ally Kamwe awatupia dongo hili watani zao Simba hii ni baada ya kushinda mechi ya Jana dhidi ya Monastri


Afisa Habari wa Yanga Ally Kamwe

Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA

Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kikosi cha timu hiyo kimetoa somo namna ya kuzifunga timu kutoka Kaskazini mwa Afrika (Waarabu).

Kamwe ametoa kauli hiyo baada ya Yanga kuitungua US Monastir ya Tunisia kwa bao 2-0 katika Dimba la Mkapa na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

“Yanga tumetoa somo zuri ya jinsi gani ya kumfunga mwarabu nyumbani kwako. Kama kuna timu inataka kuchukua hili somo download mechi yetu dhidi ya Monastir kisha utanikumbuka baadae.

“Hakikisha mnapoangalia na nyie mna striker kama Musonda, kama striker wako anapiga kichwa kama kondoo usijishuhhulishe kuangalia,” amesema Kamwe.

Ikumbukwe pia kuwa, Yanga iliifunga Clube Africain ya Tunisia katika hatua ya mtoano na kufanikiwa kutinga hatua ya Makundi ya Kombe hilo.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz