SAMIA anunua magoli ya Simba na Yanga wiki hii

SAMIA anunua magoli ya Simba na Yanga wiki hii

SAMIA anunua magoli ya Simba na Yanga wiki hii

SAMIA anunua magoli ya Simba na Yanga wiki hii

SAMIA anunua magoli ya Simba na Yanga wiki hii

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Hassan Suluhu ametangaza kulinunua kwa Tsh. Milioni 5 kila goli litakalofungwa na Simba au Yanga katika michezo yao inayochezwa wiki hii wakiiwakilisha Tanzania kwenye Michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwa Simba SC na Kombe la Shirikisho Afrika kwa kwa Yanga.

Taarifa hiyo imetolewa kwa Wahariri na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa leo Jijini Dar es salaam ambapo amenukuliwa akisema “Rais Samia amenituma niseme kuwa kila goli litakalofungwa na Simba au Yanga atainunua kwa Tsh. Milioni 5”

“Kazi kwenu Wachezaji ukifunga magoli mawili una Tsh. Milioni 10, lengo lake pamoja na kufunga magoli Timu zetu lazima zishinde kwenye michuano hii”

Simba SC ni Wawakilishi wa Tanzania katika michuno ya Klabu Bingwa Barani Afrika ambapo watacheza dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco Jumamosi hii ya February 18 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, wakihitaji ushindi ili kufufua matumaini ya kuvuka hatua ya Makundi katika Kundi C na kutinga robo Fainali.

Yanga SC wao wanacheza Jumapili hii ya February 19 dhidi ya Mkapa dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, wakihitaji ushindi ili kumaliza nafasi mbili za juu katika Kundi D Kombe la Shirikisho na baadae kukata tiketi ya kutinga robo Fainali.

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

DONWLOAD NIJUZE TV HAPA SISI kwetu Michezo ndiyo Furaha YETU.

The post SAMIA anunua magoli ya Simba na Yanga wiki hii appeared first on Nijuze Mpya.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post