Sababu za Saido kubaki Dar zatajwa - EDUSPORTSTZ

Latest

Sababu za Saido kubaki Dar zatajwa

Sababu za Saido kubaki Dar zatajwa

Sababu za Saido kubaki Dar zatajwa

Sababu za Saido kubaki Dar zatajwa

Sababu za Saido kubaki Dar zatajwa

Klabu ya Simba SC, leo alfajiri imesafiri kuelekea nchini Guinea kwaajili ya mchezo wa kwanza wa kundi C Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Horoya Athletic Club.

Mchezo huo unatarajiwa kufanyika Jumamosi ya February 11, 2023 kuanzia saa 1:00 Usiku kwenye Uwanja wa General Lansana Conte.

Kuelekea mchezo huo Simba itaikosa huduma ya Kiungo wao Mshambuliaji, Saido Ntibazonkiza ambaye hakuwa sehemu ya Kikosi kilichoifuata Horoya AC.

Baada ya kumtafuta Daktari wa Simba, Edwin Kagabo amesema kuwa Saido anaendelea vizuri na killichomfanya kutokuwa kwenye kikosi kinachosafiri ni kutokana na kutofanya mazoezi pamoja na wenzake.

Kagabo amefafanua kuwa Saido alipata maumivu ya nyama za paja katika mchezo dhidi ya Singida Big Stars, na hali yake imeimarika lakini hawezi kusafiri kwa kuwa hayuko timamu na hajafanya mazoezi na wenzake.

Daktari huyo ameongeza kuwa timu hiyo ikirejea nchini Saido atajiunga na Wachezaji wenzake kwaajili ya maandalizi ya michezo inayofuata.

Baada ya kurejea nchini Klabu ya Simba itaanza maandalizi ya mchezo wa pili wa Kundi C dhidi ya Raja Casablanca utakaopigwa February 18, 2023 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

DONWLOAD NIJUZE TV HAPA SISI kwetu Michezo ndiyo Furaha YETU.

The post Sababu za Saido kubaki Dar zatajwa appeared first on Nijuze Mpya.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz