MATOKEO Simba Queens vs Determine Girls 02 November 2022
Timu ya Simba Queens imefanikiwa kuibuka na Ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Determine Girls ya Liberia kwenye mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Women’s Champions League)
Bao la kwanza la Simba lilifungwa na Mshambuliaji wake, Opa Clement dakika ya 53 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Olaiya muda mfupi baada ya kuingia.
Bao la pili na la ushindi lilifungwa na Olaiya kwa mkwaju wa penati dakika ya 79 baada ya Joelle Bukuru kufanyiwa madhambi ndani ya 18.
Simba Queens inatarajiwa kucheza mchezo mwingine wa mwisho wa hatua ya makundi Jumamosi hii ya November 05 dhidi ya Green Buffaloes ya Zambia.
Baada ya Ushindi huo, Kocha Mkuu Charles Lukula, alisema kuwa kilichofanikisha kupata Ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Determine Girls ni kuwajenga kisaikolojia Wachezaji wake baada ya kucheza kwa presha kipindi cha kwanza.
Lukula alisema kuwa kipindi cha kwanza walipoteza nafasi nyingi ambazo ziliwafanya kucheza kwa presha na kufanya makosa kadhaa.
Lukula aliongeza kuwa baada ya kwenda mapumziko alizungumza na wachezaji na kuwaambia watulie na kucheza kawaida na hicho ndicho kilichosababisha tupate ushindi.
“Ni furaha kwangu kupata ushindi wa kwanza kwenye michuano mikubwa hii, tulicheza vizuri lakini tulipoteza nafasi nyingi kipindi cha kwanza na kutufanya kucheza kwa presha,” amesema Lukula.
Taarifa zaidi za mchezo huo bofya HAPA.
The post MATOKEO Simba Queens vs Determine Girls 02 November 2022 appeared first on Nijuze Mpya.
No comments:
Post a Comment