CLUB Africain yafanyiwa vurugu kwa Mkapa - EDUSPORTSTZ

Latest

CLUB Africain yafanyiwa vurugu kwa Mkapa

CLUB Africain yafanyiwa vurugu kwa Mkapa

CLUB Africain yafanyiwa vurugu kwa Mkapa

CLUB Africain yafanyiwa vurugu kwa Mkapa

CLUB Africain yafanyiwa vurugu kwa Mkapa

KLABU ya Young Africans huenda ikakumbana na adhabu kutoka Shirikisho la soka Barani Afrika CAF, kufuatia vitendo visivyo vya kiungwana walivyofanyiwa baadhi ya maafisa wa Club Africain ya Tunisia.

Vitendo hivyo vimetokea kabla ya kuanza kwa mchezo wa Mkondo wa Kwanza uliopigwa November 02,2022 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.

Kwa kuthibitisha ushahidi kwanjia ya Video, Club Africain imeweka Video ya vitendo walivyofanyiwa maafisa wake wakati wakiwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, inayoonyesha maafisa hao wakimwagiwa maji na Makomandoo wa Young Africans na kuzuiliwa kuingia katika moja ya vyumba vya Uwanja huo.

Video Club Africain yafanyiwa vurugu kwa Mkapa

Video hiyo iliyowekwa katika ukurasa wa Facebook wa Club Africain ilikuwa ikirushwa Mubashara, kwa makusudi ya kuuonyesha umma yale yaliyotokea Uwanja hapo dakika kadhaa kabla ya mchezo huo kuanza.

Mbali na kuweka video hiyo, Club Africain imerikodi matukio yote waliyokutana nayo kabla na baada ya kufika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Hata hivyo CAF ndio wenye maamuzi ya mwisho endapo Club Africain watawasilisha malalamiko ya kufanyiwa vitendo hivyo walipokua Uwanja wa Benjamin Mkapa na kuyatolea maamuzi kwa mujibu wa Ripoti ya Msimamizi mkuu wa mchezo huo wa Mkondo wa Kwanza.

The post CLUB Africain yafanyiwa vurugu kwa Mkapa appeared first on Nijuze Mpya.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz