YUSSUF BAKHRESA AMEAMUA, ASHUSHA MUIVORY COAST MWINGINE AZAM -Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

YUSSUF BAKHRESA AMEAMUA, ASHUSHA MUIVORY COAST MWINGINE AZAM -Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL Ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako nakutasoma habari zote hata kama hauna MB

KLABU ya Azam FC imetambulisha mchezaji mwingine kutoka Ivory Coast, naye pia kiungo mshambuliaji, Tape Edinho aliyesaini mkataba wa miaka mitatu.
Azam FC imemnunua Edinho tumemnunua kutoka ES Bafing ya kwao, ambapo mkataba huo utamfanya kuhudumu ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2025.
Usajili wa nyota huyo mwenye uwezo mkubwa umekamilishwa na Mkurugenzi timu, Yusuf Bakhresa akishirikiana na Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat'.
Mkali huyo amechaguliwa kwenye kikosi bora cha Ligi Kuu ya Ivory Coast (Ligue 1) msimu huu, kutokana na ubora wake wa kuhenyesha wachezaji wa timu pinzani.
Msimu uliomalizika, amefanikiwa kufunga jumla ya mabao matano na kuchangia pasi tisa zilizozaa mabao.
Anakuwa Muivory Coast wa pili kutambulishwa leo baada ya 
Kipre Junior Zunon kutokea Sol FC ya kwao pia ambaye naye amesaini mkataba wa miaka mitatu.







Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz