MECHI za mchujo wa kuwania kubaki Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina ya Mtibwa Sugar na Tanzania Prisons zutachezwa Jumapili na Jumatano, Julai 6.
Mechi ya kwanza itachezwa Jumapili Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, Tanzania Prisons wakiwa wenyeji na marudiano na Jumatano Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro Mtibwa wakiwa wenyeji.
Timu itakayoshinda itabaki Ligi Kuu na itakayofungwa itakwenda kumenyana na JKT Tanzania kutoka Championship na mshindi ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.
Mechi dhidi ya JKT Tanzania zimepngwa kucheza Julai 9 Uwanja wa Meja Isamuhyo huko Mbweni, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na marudiano Julai 13 Sokoine au Manungu.
No comments:
Post a Comment