MSHAMBULIAJI chipukizi wa Yanga, Clement Francis Mziza amekuwa mchezaji wa kwanza kupiga hat-trick kwenye Ligi ya Vijana chini ya umri wa miaka 20.
Nyota huyo alifunga mabao yote matatu akiisaidia timu yake kushinda 3-1 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wao wa kwanza wa Kundi D usiku wa jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Mechi nyingine ya Kundi D jana, KMC ilitoa sare y 1-1 na Kagera Sugar, wakati Kundi B, Mbeya Kwanza iliichapa 3-1 Ruvu Shooting na mabingwa watetezi, Mtibwa Sugar wakaitandika 4-0 Dodoma Jiji.
Michuano hiyo ilianza juzi, Kundi A; Biashara United ikitoka sare ya 0-0 na Namungo FC na Simba SC ikaichapa Polisi Tanzania 2-1, wakati Kundi C, Tanzania Prisons iliichapa Coastal Union 1-0 na wenyeji, Azam FC wakaichapa Mbeya City 3-2.
No comments:
Post a Comment