Dare es Salaam. Shirika la Umeme nchini (Tanesco) limesema wateja wa huduma ya ununuzi wa umeme kupitia Luku watakosa huduma hiyo kwa saa mbili kwa usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi Juni 9 mwaka huu.
Huduma hiyo itakosekana kuanzia saa 6 usiku hadi saa 8 usiku nchi nzima ili kupisha maboresho ya mfumo wa manunuzi ya umeme kwa wateja wanaolipia kabla ya matumizi (Luku), kupitia mifumo iliyopo katika kituo cha kujikinga na majanga (Disaster Recovery).
Akizungumza leo Juni 06/2022 kwenye makao makuu ya taasisi hiyo, Meneja Mwandamizi wa Tehama, Cliff Maregeli amesema kutokana na changamoto hiyo ya kiufundi wateja wanashauri kununua umeme wa ziada ili kuepuka usumbufu ambao unaweza kujitokeza.
"Maboresho ni muhimu na yanalenga kuongeza ufanisi kwenye mfumo wa manunuzi ya umeme ili kuhudumia wateja wengi ipasavyo pale inapotokea hitilafu ya aina yeyote katika kituo chetu Kikuu Cha mfumo," amesema Maregeli
Kwa uapande wake Msemaji wa Shirika hilo, Martini Mwambene ameshauri wateja kuzingatia taarifa hiyo ili kuruhusu maboresho hayo ya mfumo kufanyika.
No comments:
Post a Comment