TIMU za taifa za Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya michuano ya CECAFA Challenge baada ya ushindi wa 12-0 dhidi ya Zanzibar, Zanzibar Queens jana Uwanja wa FUFA Technical Centre, Njeru katika mechi ya mwisho za Kundi B.
Mabao ya Kilimanjaro Queens yalifungwa na Opa Clement manne, Janeth Pangamwene, Diana Msewa, Enekia Kasonga ‘Lunyamila’, Mwanahamisi Omar ‘Gaucho’ matatu, Protas Mbunda na Ester Mabanza.
Mechi nyingine ya mwisho ya Kundi B, Ethiopia iliichapa Sudan Kusini 4-0 hapo hapo FTC Njeru.
Sasa Kilimanjaro Queens itamenyana na Burundi katika Nusu Fainali Alhamisi, wakati Ethiopia itawavaa wenyeji, Uganda, wakati Zanzibar na Sudan Kusini zinaungana na Rwanda na Djibouti za Kundi A kuyaaga mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment