Romelu Lukaku Akamilisha Dili la Kurudi Tena San Siro kwa Mkopo-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Romelu Lukaku Akamilisha Dili la Kurudi Tena San Siro kwa Mkopo-Michezoni leo

Romelu Lukaku amefunga mabao 8 katika mashindano ya Ligi Kuu ya Uingereza

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Chelsea Romelu Lukaku amekamilisha dili la kurudi katika viunga vya klabu yake ya zamani ya Inter Milan kwa mkataba wa mkopo wa msimu mmoja.

 

Kiasi cha ada kinachodaiwa kulipwa na Inter Milan ni pauni milioni 8 ambapo Chelsea wanatajwa kutohusika tena na malipo ya mshahara wa Lukaku kwa msimu mzima.

Romelu Lukaku akiwa ndani ya uzi wa Inter Milan

Habari za ndani zinadai kuwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu hiyo ambaye ametangazwa rasmi kutimka klabuni hapo Bruce Buck pamoja na Mkurugenzi wa Utendaji mwanamama Marina Granovskaia walitaka kumbakiza Lukaku kwa msimu mmoja zaidi abaki klabuni hapo ili kuona ni kwa namna gani anaweza kurekebisha kiwango chake, lakini mmiliki mpya Todd Boehly alikuwa na mawazo tofauti na akaamua kumtoa kwa mkopo kurudi Inter Milan.

Moja ya sababu ya kupotea kwa Lukaku ni majeruhi aliyoyapata mwanzoni mwa msimu

Kwa mujibu wa Matt Law ambaye ni mwandishi wa habari wa gazeti la Telegraph anadai hisia ndani ya klabu hiyo ni kwamba Romelu Lukaku anaweza kutolewa kwa mkopo wa msimu mwingine wa 2023/2024 au kuuzwa jumla.

 

Romelu Lukaku amekuwa na moja ya msimu wa kupanda na kushuka kwani alianza kwa kasi akifunga mabao matatu kwenye michezo miwili kabla ya kukubwa na majeraha pamoja na Covid-19 ambavyo vilimuondoa kwenye kiwango chake alichoanza nacho, amefanikiwa kufunga mabao 15 kwenye michezo 44 aliyocheza akiwa na uzi wa Chelsea huku mabao 8 kati ya hayo akifunga kwenye mashindano ya Ligi Kuu ya Uingereza.

The post Romelu Lukaku Akamilisha Dili la Kurudi Tena San Siro kwa Mkopo appeared first on Global Publishers.





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz