Mrembo mmoja toka Lagos nchini Nigeria, Crystabel anadaiwa kufariki katika Hospitali alikokuwa amekwenda kufanya upasuaji wa kuuboresha mwili wake (plastic surgery) uwe na muonekano unaovutia zaidi.
Rafiki wa mrembo huyo, Posha kupitia Twitter ameandika; "Nataka kueleza hadharani, Rafiki yangu alifariki katika hospitali hii huko Lagos Nigeria, siku chache zilizopita. ambapo alifanyiwa upasuaji.
"Sasa mimi sipingani na mtu yeyote anayetaka kuongeza mwili wake au kitu chochote kama hicho, ni maisha yako ya mwili na ni chaguo lako, kwa hivyo fanya kile unachopenda lakini ninapingana na Madaktari wanaodai kuwa wana uzoefu kutoka nje ya nchi, wamekuja Nigeria kuua vijana wa watu.
"Baada ya upasuaji alilalamika kutokwa na damu na madaktari walidai ni kawaida, itakoma. sasa tatizo ni hili, vipi wewe ni Daktari bingwa wa plastic surgery mwenye ujuzi wa hali ya juu na mwenye uzoefu kutoka nje ya nchi na ukimaliza kumfanyia upasuaji mtu akalalamika damu ukasema ni kawaida itakoma?
"Hospitali haikuona umuhimu wa kuwasiliana na jamaa yake yeyote mpaka marafiki wachache waliojua anaenda kufanyiwa upasuaji waliposema alitakiwa kuwa amerudi, waliamua kwenda Hospitali kumchungulia; walipofika, walipewa barua kwamba mwili wake umewekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti. Hii inasikitisha". - ameeleza Posha kwenye mfululizo wa tweet zake.
No comments:
Post a Comment