Mwandishi wa Habari Raia wa Uingereza Apotea Kwenye Msitu wa Amazon - EDUSPORTSTZ

Latest

Mwandishi wa Habari Raia wa Uingereza Apotea Kwenye Msitu wa Amazon



MWANDISHI wa Habari mkongwe raia wa Uingereza Don Philips akiwa pamoja na mwenyeji wake Bruno Araujo Pereira ambaye ni mtaalam wa masuala ya misitu kutoka nchini Brazil wamepotea katika msitu wa Amazon

Taarifa za kupotea kwao zimetoka baada ya kupoteza mawasiliano ya Satelite kwa muda wa masaa 30 tangu walizama kwenye msitu mnene wenye mito mingi ndani ya bonde la Javari.


Msitu wa Amazon unasifika kwa kuwa msitu menene na wenye mito mingi
Tayari Mamlaka ya Uokoaji na Uchunguzi ikishirikiana na Jeshi la Polisi imetuma timu mbili za uokoaji katika eneo hilo ambalo lina changamoto ya kupitika.

Gavana wa Jimbo la Amazona Wilson Lima ameagiza kuongezwa kwa idadi ya askari waokoaji ili kuhakikisha zoezi hilo la uokoaji linakamilika kwa wakati.


 
Hofu imetanda kuwa kuna uwezekano watu hao wakawa wameuawa na makundi ya watu wanaoishi msituni mo kwani taarifa zinadai mwaka 2019 Maxciel Pereira Dos Santos aliuawa katika mazingira hayohayo.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz